UJENZI WA BARABARA-ARUSHA


Mpini Wa Shoka unakukumbusha tu kwamba pamoja na sehemu kubwa ya barabara za katikati ya Mji wa Arusha zimekwisha kuwekwa lami na zinapendeza kwelikweli, lakini baadhi bado zinaendelea kushughulikiwa kwa umakini na jamaa zetu wa Ki-china. Kama barabara hii ya Njiro-Arusha ambayo inaanzia Njiro katika eneo linalofahamika kama mwisho wa lami kuelekea maeneo ya Corona, kwa sasa ndio imeingia katika hatua mpya ya kuanza kuwekewa lami ya mwanzo (tabaka la mwanzo). Kwa hivyo, muda siyo mrefu sana nayo itakuwa tayari imekamilika. Kwa hakika hongereni sana Wa-Chainiz. (Picha zote kutoka maktaba)

No comments: