UKITAKA KUFANYA KAZI YA GEREJI NI LAZIMA UCHAFUKE...
Mpini Wa Shoka ulipita eneo maarufu mjini Arusha linalofahamika kama Unga Limited. Mpini ukaingia ndani na mojawapo ya gereji nyingi za magari zilizopo katika eneo hili, ambalo pia ni eneo maarufu kwa viwanda na karakana ndogondogo. Hapa ndani ya gereji hii ni kazi tu kwa kwenda mbele....
Hakuna kuchagua mahali pa kulala au kukaa... Ni popote tu, ilimradi kazi ya mteja ifanikiwe kwa kiwango kinachostahili.
Hawa wao wanahangaika ili kuhakikisha gari hili linakwanguliwa vizuri kila mahali, kabla ya kuanza kazi ya kulipiga rangi...
Compresa kwa kazi ya upigaji rangi magari nayo iko tayaritayari...
Huyu ni mmoja wa mafundi waandamizi katika gereji hii, maarufu zaidi kwa jina la Bwana Kipara. Spana zake mkononi tayari kwa kazi. Hapa alikuwa akinionesha kwa mzaha tu ni kwa jinsi gani fundi mlevi anavyoweza kuonekana alivyo wakati wote kwa siku nzima katika eneo lake la kazi...
No comments:
Post a Comment