NDANI YA OLD MOSHI SEKONDARI

Kuna mambo yamenibana kidogo ndio maana nimeshindwa kukurushia vitu mfululizo. Usikonde. Alhamisi ya wiki hii Mpini Wa Shoka ulikuwa ndani ya Mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro, ukiwa umealikwa katika sherehe za maafali ya 49 ya kidato cha 6 katika shule ya sekondari ya Moshi (Old Moshi Sec.) Leo nakuonjesha kidogo tu, halafu kesho nitajitahidi kukumwagia mapicha kibao ya shughuli hiyo na vimbwanga vyake kedekede....

Mojawapo ya mizunguko maarufu ya magari (keepleft) katika Mji wa Moshi wakati tukielekea Old Moshi Sec (Picha na Khadija Abdallah)






Hapa ni ndani ya eneo la shule






Kwa sababu ilikuwa ni siku ya maafali, basi wajasiliamali nao hawakukosa cha kuuza na hasa maua na kadi kama hizi 





Waalimu na watumishi wengine wa shule hii wakijadiliana jambo kabla ya kuelekea kwenye viwanja vya maafali 






Haya ni baadhi tu ya mabweni na madarasa ya wanafunzi kama yanavyoonekana 






Hii ni sehemu ya wahitimu wenyewe wa kidato cha 6 wakiandamana kwa raha kuelekea kwenye viwanja vya maafali 




HAPA NDIPO KWENYE VIWANJA VYA MAAFALI vilivyopo ndani ya eneo la shule...





 

Waalimu na watumishi wengine wa shule wakiwasili kwenye meza kuu...

Waliovaa miwani mstari wa mbele ni waalimu wasioona (walemavu wa macho)

No comments: