Jamaa anasubiri usafiri (kushoto), sijui hata anataka kwenda wapi! Lakini alichonifurahisha ni jinsi alivyouwekea ulinzi wa kutosha mzigo wake. Yawezekana hapa hana hata mtu mmoja anayemwamini; kwa hivyo, kwa ajili ya kuhakikisha usalama zaidi, ameona ni heri abaki na mzigo wake kichwani hadi pale usafiri utakapofika au ikibidi apige tu kwa mguu hadi huko anakokwenda...! Mambo ya Hedaru haya, hata huduma ya usafiri wa pikipiki (bodaboda) nao pia upo wa kutosha kama unavyoona hapa chini.
HAPA NI MAKANYA...
Pamoja na ustawi mkubwa wa kilimo cha zao la Katani (mkonge), ambacho kwa sehemu kubwa kinaonekana kuzorota sana hivi sasa, tofauti na ilivyokuwa kwa miaka mingi iliyopita, lakini Mji huu ni eneo mojawapo katika nchi ya Tanzania ambako panapatikana mawe ambayo hutengenezwa saruji (sementi) viwandani (baadhi yanaonekana kwenye picha yakiwa yamerundikwa). Wapo watu wengi tu ambao wameibukia kuwa matajiri wakubwa, kutokana na kujihusisha na kazi hii ya uchimbaji wa mawe haya ya kutengenezea Saruji (Sementi) hapa Makanya.
No comments:
Post a Comment