MOMBO (TANGA REGION)
Kwa muda mrefu wa miaka chungu tele sasa, kwa wasafiri wanaotumia barabara kuu ya Arusha-Dar... Arusha-Tanga, Mji wa Mombo umekuwa ndipo eneo la wasafiri kujipatia msosi (chakula). Nakumbuka zamani zile za enzi zile za Mzee J.K Nyerere na Alhaji Ally Hassan Mwinyi (Tanzanian former presidents) wakati mabasi yalipokuwa yakisafiri usiku kwa usiku, sehemu iliyokuwa ikitumika kwa kupata chakula hapa Mombo ilikuwa barabarani kabisa. Zipo hadithi nyiiiiiiiingi tu (na nyingine huenda hata ni za kizushi tu) kwamba, enzi hizo wasafiri waliwahi hata kulishwa nyama za majogoo ya kunguru na mwewe pamoja na chipsi za mayai ya bundi na ya kenge! Sasa siku hizi katika enzi hizi ambazo ni marufuku mabasi ya abiria kusafiri usiku nchini Tanzania, eneo hili la Mombo limejikuta likiota utitiri wa maeneo ya kupatia msosi kwa wasafiri! Mengine yameboreshwa hata kufanana kabisa na hoteli za kitalii! Lakini tatizo kubwa la maeneo hayo ni bei za vitu, Wakwetu! Kama mfuko wako ni mwemba kama wa kwangu, basi unaweza ukajikuta unapiga miayo tu au uamue kujipatia paketi 1 ya biskuti tu ili nyongo tumboni isije ikakujeruhi...ni hatari!
Na hili ndilo miongoni mwa maeneo mapya kabisa yaliyoibuka kama uyoga miaka ya hivi karibu tu... Wakwetu, wasafiri hapa ni kama watalii vile.
Bango linaonesha kwamba Hoteli yao ipo Kariakoo-Dar es salaam. Kwa hivyo, hapa Mombo hili ni tawi tu la hoteli hiyo.
No comments:
Post a Comment