MPINI WA SHOKA BACK TO HOME-DAR-ARUSHA.

Wakati mwingine ukiwa ndani ya chombo cha usafiri kwa safari ndefu unaweza ukajing'ang'aniza kweli ili usisinzie hata kidogo, kwa lengo la kuyaona maeneo na miji karibu yote ya njiani mnakopita, lakini wapi Wakwetu! Siri ya usingizi anayeijua kwa usahihi ni yule tu pekee aliyetuumba sisi sote na ku-uumba huo usingizi wenyewe, yaani Mwenyezi Mungu! Wakati unapokupitia, hata wewe mwenyewe haujielewi kabisa! Mpini Wa Shoka nao ukitokea Dar kurudi Arusha, usingizi haukuufanyia ajizi hata kidogo hapa na pale. Maeneo kadhaa wa kadhaa yakajikuta yakiyapita tu.... Lakini siyo sawa na kukosa kabisa... macho yalipofunguka, kazi ikaendelea...

Eneo la kupimia uzito wa magari- Wami

 



Daraja la Mto Wami; maji kibao mtoni. Habari za Mamba hapa usiulize. Wapo wa kutosha. Ukijipendekeza tu, Wakwetu utakiona cha mtema kuni!




 NJIA PANDA YA HIMO...

Ndani ya stendi ya Njia panda ya Himo. Biashara za kila rangi zinaendelea; wajasiliamali, wake kwa waume, wanajituma. Chombo cha usafiri kikiingia tu ndani ya stendi hii, basi ni mbio tu za huku na kule kwa ajili ya kuuza bidhaa hizi na zile kwa wasafiri. Kweli maisha ni mapambano na juhudi tu kwa kwenda mbele; lakini siku zote tusisahau kwamba aliyetuumba yupo katikati ya harakati na pilikapilika zetu zote. Tumwombe kwa bidii.




Mji wa Njia Panda ya Himo. Hili bango sijui hata lilikumbwa na dhoruba gani hasa, hata likachanika namna hii! Hata maelekezo yake hayasomeki tena vizuri! Yawezekana wahusika wenyewe (Tanroad) macho yao hayafanyi kazi vizuri; acha tu likae hivyohivyo, maana ukijaribu tu kusema wataanza kulalamika "oooh! unatuchongea!"





Kwenye mzani wa kupimia uzito wa magari-Njia Panda ya Himo

No comments: