WELCOME TO KIGAMBONI...KARIBU SANA.

Ingawa Mpini Wa Shoka haukuzurura katika maeneo meeeeeengi ya Mji huu kwa saaaaaana, lakini kwa ufupi ni Mji mzuri.

Mitaa na vitongoji vya Kigambonino. Si unaona mwenyewe.





Mambo ya Kigamboni haya, Yakhe! Kifuko cha nyanya mkononi..! Mkoba begani..! Sijui hata tunaelekea pande zipi hasa! Kupanda daladala hiyo iliyoko mbele yetu..! Au ndio tumeshafika maeneo ya home hapa jiranijirani tu..! Hayakuhusu na Mpini wako Wa Shoka... endelea na shughuli zako! Kuna watu hata ndani ya Jiji lenyewe la Dar es salaam wanajua kwamba Kigamboni ni Kisiwa! Ni Kisiwa kwa sababu watu hutumia usafiri wa Kivuko-ferry kutoka katika Jiji hadi Kigamboni. Yawezekana hata wewe siku zote umekuwa ukielewa hivyo. Aisee, Kigamboni siyo Kisiwa. Wakwetu, Kigamboni ni Mji uliopo katika Wilaya ya Temeke; na unaweza ukaamua kwenda Kigamboni na kurudi bila ya kuvuka kwa njia ya maji (kupanda Kivuko-ferry). Tatizo ni kwamba, kwa kutokea katikati ya Jiji itakubidi utumie muda mrefu sana kwani itakubidi uzunguke kwa barabara inayokwenda Temeke (barabara ya Kilwa) ndipo uibukie Mji Mwema-Kigamboni. Na ukichanganya tena na mambo ya msongamano barabarani (jam), ndipo itakuwia balaa tupu! Sasa kwa kuvuka na kivuko-ferry ni karibu tu. Ni kama mwendo wa kusukutua tu mdomo! Yaani ni faster.





Mpini Wa Shoka ulifika hadi ndanindani kidogo kwenye makazi ya wenyeji...





Nyumba za ibada, misikiti, makanisa na kadhalika, nazo zipo nyingi tu kama hivi unavyoona... kazi ni kwako. Welcomen to Kigamboni... Karibu sana.

No comments: