AJALI!

Ni muda wa asubuhi; wastani wa kama saa mbili hivi ya siku ya J'4 ya tarehe 12/02/2013, wakati watu wengi wakiwa katika pilikapilika za kuwahi katika maeneo yao ya kazi, ndipo Mpini Wa Shoka ukakutana punde tu na tukio hili eneo la OilCom-Sakina. Mwanamama dereva wa gari hili alikuwa akijaribu kumwepuka mwendesha pikipiki (bodaboda) ndipo kikatokea hiki....

Gari likamshinda akajikuta anaingia katika upande wa barabara usiokuwa wa kwake na kutumbukia kwa kishindo ndani ya mtaro huu uliopo pembezoni kabisa mwa kituo cha mafuta cha OilCom



Wananchi wakiwa wamemzunguka kila upande dereva wa gari hili (mwanamama aliyekaa chini katikati); akipumzika kidogo baada ya kunusurika katika ajali hii.





Ni gari namba T 845 AAL, aina ya Suzuki. Hakuna aliyekufa wala kujeruhiwa vibaya katika tukio hili, zaidi ya gari hili kuharibika upande wa mbele kama unavyoliona....

No comments: