HEKAHEKA ZA KILIMO KWANZA BADO ZINAENDELEA...

Hiki ni kituo kingine cha utayarishaji wa mbegu bora. Kipo ndani ya Viwanja vya Maonesho ya Kilimo na Mifugo (TASO), maarufu kama Viwanja vya Nane Nane)-Themi Hill, Njiro-Jijini Arusha....Mpini Wa Shoka ulizurura hapa pia...

Ofisi kwa mbele




Ghala la Mbegu





Uchambuzi wa mwanzo wa kuondoa mawe na takataka zingine ndani ya mbegu




Sehemu ya wakina mama ambao ni wafanyakazi wa kitengo hiki wakiwa katika pilikapilika mbalimbali ndani ya ghala mbegu 





Baada ya upembuzi wa takataka na mawe, mbegu huletwa katika mtambo huu kwa ajili ya kufanyiwa usafi zaidi





Kisha, baada ya kutoka kwenye mtambo wa usafi, mbegu huingizwa kwenye mtambo wa kuziwekea dawa ya kuzuia wadudu kuziharibu (mtambo uliopo katikati uliobanwa na magunia meupe zaidi)





Halafu ndipo zinaletwa kwenye mtambo huu unaoonekana nyuma ya mwanadada huyu kwa ajili ya kufungashwa (parking), tayari kuwaendea wakulima



Magunia yaliyofungwa na kupangwa, ni mbegu ambazo tayari zimekwishafungashwa. Ndani ya kila gunia, kuna paketi ndogondogo zenye uzito wa kuanzia kilo 2 na zaidi 





Huyu ni mmoja wa Mawakala wa pembejeo za Kilimo na Mifugo wa eneo la Midawi, Arusha Vijijini akiwa ndani ya ghala hili kwa ajili ya kujipatia mbegu...

No comments: