JUU MLIMA MERU-ARUSHA

Ni mahali panapovutia sana kwa hali ya hewa na uoto wake wa asili pamoja na ule wa kutengenezwa na wenyeji wa maeneo haya. Hapa Mpini Wa Shoka ulifika katika eneo linalojulikana kama Shiboro-Sambasha katika wilaya ya Arusha Vijijini. Hebu na wewe tembelea kidogo... 

Makazi na vibanda vya mifugo vya wenyeji



Safu za miporomoko na miteremko mikali ya kuvutia.





Tazama ukungu kwenye kilele cha Mlima Meru. Kwa macho ukiwa hapa Shiboro, unaweza kabisa kudanganyika kwamba unaweza hata ukatembea tu kwa muda mfupi na ukakifikia kilele hiki; lakini ni hatari. Macho yanaweza yakakuponza ukajuta!





Wakati unapanda kuelekea maeneo ya Shiboro, basi njiani utakutana tu na mabango kama haya

No comments: