UTAMU WA HARUSI!
Kwa hakika, harusi ni tamu mno. Tena pale ndugu, jamaa, marafiki na hata majirani wa pande zote mbili wanapohudhuria. Lakini sijui baada ya kukamilika kwa utamu huu, tatatizo linakuwa wapi hasa! Miezi kadhaa tu baadaye, mara patashika zinaanza kwa wale waliooana hivi karibuni! Tatizo ni nini? Ni maandalizi hafifu ya ufahamu wa suala la ndoa kwa wanandoa! Ni wazazi na walezi wa wanandoa! Au ni ahadi za uongo baina ya wanandoa zinapokuwa hazitekelezeki!
Hii ni moja ya harusi za hivi karibuni iliyofanyika katika Mji wa Ngaramtoni ya chini jijini Arusha. Mpini Wa Shoka haukuwa mbali. Hebu na wewe onja kidogo Utamu wa Harusi
"Haloo, Vipi! Mbona wewe haujahudhuria hadi muda huu! Sisi tayari tuko hapa ndani ya utamu wa harusini; hebu jitahidi uwahi kuja"
Kabla ya ndoa kufungishwa, kwanza mjadala kidogo wa mashauriano
Bwana Harusi(kushoto) na mpambe wake katika pozi la kujiandaa kujichotea mke
Ndoa inafungishwa kwa kiapo. Bwana fulani bin fulani umekubali kumuoa binti fulani wa fulani kwa mahari yake ya ...... Ndiyo, nimekubali!
Mashuhuda nao hawako mbali, wanashuhudia.
Chumbani; mwanamwali akafuatwa. Haya, na weye fulani binti fulani umekubali kuolewa na bwana fulani bin fulani kwa mahari yako ya...... Ndiyo, nimekubali! Haya weka saini yako hapa kwenye cheti cha ndoa ili kukithibitisha kiapo chako
Wakati mwanamwali akiapishwa chumbani, maneno ya Mwenyezi Mungu yanasomwa hadharani kwa ustadi
Macho yanashuhudia kila pembe na kila upande...
No comments:
Post a Comment