MAISHA NI KAZI; SIYO POROJO TUPU.


Mpini Wa Shoka ulimfuma fundi huyu maarufu wa nguo za mitindo ya kila aina katika mtaa maarufu wa Jamhuri (Jaluo) jijini Arusha, Bwana Shemdaga, akiwa katika pozi la kuwajibika vilivyo kikazi zaidi akiishughulikia kwa utulivu mojawapo ya nguzo za wateja wake. Sielewi kama namba kubwa zinazoonekana kulia mwa fundi huyu ndizo bei za mashono kwa ajili ya wateja wake, au la! Aliyesimama pembeni yake ni kijana Mustafa(Musti) muuzaji wa duka la vifaa vya umeme katika mtaa huu.





Huyu ni fundi seremala; Mpini Wa Shoka pia katika mtaa huu wa Jamhuri (Jaluo) ulimnasa kijana Ochieng(Ochan) mwenye fulana ya rangi ya njano na kijana wake (kulia) akiwa ofisini pake, akiwajibika ipasavyo akipambana kuiranda vema mbao hii kwa ajili ya maandalizi ya mojawapo ya kazi za wateja wake kutoka pande mbalimbali za jiji la Arusha. Kwa hakika, maisha ni kazi; siyo mbwembwe na porojo tupu tu za mdomoni. 





Hili ni sanduku la kutunzia vifaa vya kazi (tools box) katika ofisi ya ufundi useremala ya kijana Ochieng (Ochan) pamoja na wenzake kadhaa. Unaonaje? Vifaa vimetimia, au unatamani kuwaunga mkono kwa kuwaongezea zaidi? Wanakukaribisha.



No comments: