UNAIKUMBUKA VEMA NAFSI YAKO?
Kila mara Mpini
Wa Shoka kwa hakika umekuwa ukikukumbusha juu ya kuikumbuka nafsi yako,
kabla ya dakika yako ya kifo haijakufikia kwa ghafla wakati ukiwa bado haujajiandaa
kwa lolote lile la maana la kujisaidia na kujitetea mbele ya yule aliyekuumba,
Mwenyezi Mungu. Jana mchana Mpini Wa
Shoka ulikuwa kwenye makaburi ya Njiro, nje kidogo ya Jiji la Arusha, kwenye
mojawapo ya mazishi yaliyokuwa yakifanyika kwenye viwanja vya makaburi haya…
Umati wa watu uliohudhuria ulikuwa ni mkubwa mno….
Hata vyombo vya usafiri vilivyousindikiza mwili
wa marehemu vilikuwa ni vingi, vikiwa vimeyabeba makundi makubwa ya
wasindikizaji, wakiwemo ndugu, jamaa na marafiki…
Haya ni sehemu ya makaburi ya muda mrefu ambayo
baadhi yake bado yamesaliwa na mashada ya maua
kwa juu yake…
Hiki siyo kibanda cha wavu; wala siyo mtambo wa
aina yoyote ile. Hili ni mojawapo ya makaburi yaliyojengewa na kuzungushiwa
urembo pamoja na uzio.
Hili ndilo kaburi alimolazwa marehemu (dada)
niliyefika kuhudhuria mazishi yake, ambapo baadhi ya ndugu na jamaa waliamua
wapate japo picha tu za ukumbusho.
Haijalishi umri! Na wengine pia ndipo wakapata fursa ya kupiga
picha kwenye makaburi ya ndugu na jamaa zao waliozikwa siku, miezi au miaka mingi
iliyopita.
Rafiki ndugu yangu, hebu sikia japo kidogo maneno haya ya Mpini Wa Shoka: Kama mwenyewe Mungu aliyeumba kila kitu kinachoonekana kwa macho na
hata vile visivyoonekana kabisa, ndiye aliyeahidi kwamba kila chenye nafsi
ni lazima kitaonja umauti, ni kwa vipi
wewe unajipumbaza na kujizuibaisha tu na mambo ya dunia hii na hasa yale
yasiyompendeza wala kumvutia kamwe huyo aliyekuumba, wakati ahadi yako iko wazi
tu ndani ya ahadi yake! Acha kujidanganya; jitambue mapema kuanzia sasa, kabla
sekunde ya ahadi yako haijakufikia kwa ghafla tu. Na wala usisahau kamwe
kwamba, hata kama utazikwa na kundi kubwa la watu wote wa dunia hii, lakini
bado kaburini utabaki peke yako tu. Hakuna atakayekubali kubaki nawe milele!
Kila mmojawao atarejea nyumbani kuendelea na harakati zake, akiwemo hata yule
mpendwa wako saaaaaaaaaaaaana aliyekuwa akilia na kujigaragaza ovyo huku na
kule kwa ajili ya kifo chako! Akili
kichwani mwako.
No comments:
Post a Comment