TIMU YA VIJANA WA TRANSCRAP YA MTAA WA JAMHURI MJINI ARUSHA YASAFIRI HADI MJI WA MOSHI MKOANI KILIMANJARO KWA MECHI YA KIRAFIKI YA UJIRANI MWEMA NA TIMU YA MAAFANDE WA MAGEREZA-MOSHI, AMBAO NI WASHINDI WA PILI WA LIGI YA WILAYA YA MOSHI...
Ilikuwa ni siku ya Jumapili ya tarehe 19/05/2013. Mpambano huu mkali ulifanyika kwenye viwanja vya Shule ya sekondari ya Ufundi Moshi (Moshi Technical). Vijana wa timu ya Transcrap ya Arusha wakakubali kichapo cha mabao 3-2.
Kikosi cha Transcrap katika picha yapamoja kabla ya pambano kuanza
Wakipasha misuli moto na kunyoosha viungo hapa na pale kabla ya kutumbukia dimbani
Mkongwe (kushoto) ambaye pia niliwahi kusukuma naye kabumbu wakati fulani katika ligi ya Mkoa wa Arusha, Ramadhani Abdulkadir 'Kaluluu' enzi zetu tukimfananisha na mshambuliaji hatari wa pembeni wa timu ya taifa ya Zambia, marehemu Moses Chikwalakwala, naye pia alikuwepo mjini Moshi katika mpambano huu. Hapa akiipasha misuli moto pamoja na mshambuliaji hatari chipukizi mwenye bukta nyekundu, Fred
Walinda mlango wa Timu hii ya Transcrap nao hawakuacha kujipasha moto vilivyo...
Dua na maombi ya pamoja kabla ya mechi
Shughuli ikaanza dimbani...
Ilikuwa ni hekaheka na patashika tupu; nguo kuchanika...
Wachezaji wa akiba na viongozi wa Transcrap wakiwa wametulia wakiufuatilia mpambano kwa makini...
Ni mapumziko. Transcrap wakiwa tayari wako nyuma kwa bao 3...
Wanajadiliana jambo kabla ya kutoka uwanjani kwenda kupumzika...
"Tukirudi kipindi cha pili tunakwenda kufanya nini? Makosa yetu yako wapi hasa hadi sasa tukiwa tumekwishapwa bakora 3," Vijana wakijaribu kupanga mikakati
Kipindi cha pili. Timu zinarejea uwanjani kwa ngwe ya mwisho...
Sehemu ya washabiki na wapenzi wa timu zote mbili kutoka Arusha na Moshi, waliofika uwanjani kulishuhudia pambano...
Pambano limekwisha. Giza limekwishaingia. Sasa nikurejea tu nyumbani tukajipange upya baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-2...
Mchezaji wa kiungo Khamis Mkwizu (mwenye bukta ya bluu) akisisitiza jambo kwa uchungu mbele ya wachezaji wenzake wa Transcrap wakati wakibadilisha mavazi tayari kwa safari ya kurejea Arusha.
(Picha zote kwa hisani ya wachezaji na viongozi wa timu ya transcrap ya Arusha-shukurani sana)
No comments:
Post a Comment