NDULA (VIATU) JUU KABISA KWENYE NYAYA ZA UMEME!


Kama ni kuvaliwa, basi mwenye viatu hivi alistahili kupewa japo hata kaji-zawadi kadogo tu na wenye kiwanda kilichovitengeneza viatu hivi, kwa jinsi alivyovitumia kisawasawa hadi kuvifikisha katika hali hii vinavyoonekana navyo! Hebu kitazame vema hicho kimoja jinsi kilivyobomoka! Unaweza ukahisi labda na vyenyewe vilikuwa kwenye hekaheka na patashika nguo kuchanika ya wananchi wa Mtwara dhidi ya jeshi la polisi, katika yale mambo yetu ya hazina ya gesi yanayoendelea kurindima nchini Tanzania! 

(Hii ni katika nyaya za umeme za Mji wa Arusha)

No comments: