MAMBO YA WACHINA HAYA, WAKWETU! KAZI YA KUZIBORESHA NA KUZITENGENEZA BARABARA ZA JIJI LA ARUSHA BADO INAENDELEA; NA TAYARI ARUSHA IMEKWISHAANZA KUMEREMETA.
Baada ya kujengwa kwa miezi kadhaa, hatimaye
daraja kubwa linalovuka mto Themi kwenye barabara mpya iliyokamilika hivi
karibuni, limeanza rasmi kazi kama unavyojionea
mwenyewe hata malori ya mizigo yameanza kulitumia. Kwa wenyeji wa Jiji la
Arusha, barabara hii imetengenezwa kuanzia eneo la round about ya Five Stars
(N.M.C) ikipita karibu kabisa na maghorofa ya polisi eneo la Faya, hadi barabara iendayo
Njiro na Kijenge jirani na hospitali ya A.I.C.C. Kama una miaka mingi haujafika
Arusha, basi chunga sana siku utaporejea usije ukafika kwenye barabara hii mpya
ukaanza kubabaika ovyo. Pia kwa sasa inaunganishwa na kipande kidogo
kinachopitia kiwanda cha bia. Mambo ya wazee wa hu ha haya-Wachina, wakwetu!
Juu ya daraja hilo na lami yake maridadi
Wenye vyombo vya usafiri wakijinafasi kwa raha zao jirani kabisa na daraja hili
Huu ni mzunguko (round about) mpya kabisa ambao haukuwepo hapa. Wachina wakaamua kufanya ubunifu wao maridadi; wakauweka hapa mzunguko huu. Ni kwenye barabara hiihii palipojengwa daraja jipya (lililopo kwenye picha za juu). Mzunguko huu unatazamana na ofisi za Zimamoto (firebrigade) upande wa kushoto mwa picha hii. Tazama kwa makini Mpini Wa Shoka ukuelekeze: upande ambako unaiona daladala (town bus) inaelekea, ni barabara ya kwenda ofisi za Tanesco, Arusha Internation School hadi Clock Tower (New Arusha Hotel). Na mbele unakoyaona magari kwa mbaaaaali, ni mwelekeo wa Five Stars (NMC). Hapa kwenye mzunguko huu mpya, wachina wameweka karibu barabara zipatazo sita! Sasa, kwa wale madereva wenzangu na mimi wasiozijua vema sheria za barabarani, hapa huwa wanapata shida kwelikweli!
No comments:
Post a Comment