TAIFA BILA MALARIA, INAWEZEKANA?


Unayaonaje mapambano dhidi ya malaria yalivyopamba moto pande hizi. Ndugu Mh. President of the country, Waziri Mkuu pamoja na Mh. Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, mnaona jinsi huku kwetu tunavyojituma kupambana na malaria, kuanzia nje ya nyumba zetu? Yaani tunawadhibiti mbu vilivyo kwa kwenda front, babaake. Ama kweli, wataalamu kuweni makini sana. Tabia ya kujisifu kwa idadi ya miche ya miti iliyopandwa, inahitajika sasa kufanyiwa marekebisho; na badala yake ni vema sana kujisifu kwa idadi ya miche ya miti iliyokubali kuota na kukua katika maeneo husika, na kujua kwa usahihi idadi ya ile iliyojifia. Wenyewe si mnajionea kwa macho yenu kazi inayofanywa na hivi vyandarua hapa mbele yenu? Hivi navyo pia vimo katika idadi ya takwimu za wataalamu wa malaria nchini kwamba viligawiwa, na vinaendelea kutimiza lengo la Taifa bila ya malaria inawezekana. Kalaghabao! Hizi ni pande za Sokoni One, jijini Arusha.



No comments: