MUDA WA SAA 12:30 HIVI ZA ASUBUHI, Mpini Wa Shoka UKIWA KATIKA SAFARI ZAKE ZA ASUBUHI ASUBUHI NDANI YA JIJI LA ARUSHA, MARA GHAFLA TU UKAKUTANA LIVE-BILA YA CHENGA NA TUKIO LA AJALI HII...
Ni kwenye barabara ya Njiro, jirani kabisa na maeneo mawili ya Tanesco na lile la Seminari, magari haya mawili yalikutana uso kwa uso. Kwa mujibu wa maelezo ya mashuhuda, mwana mama mwenye gari dogo la rangi nyeupe aliyekuwa akitokea Njiro kwa kasi akielekea pande za katikati ya Mji, ndiye aliyefanya kosa la kujaribu kuli-overtake gari jingine, na ndipo akashindwa kulimiliki gari lake na kujikuta akigongana mbele yake na basi dogo la rangi ya njano la watoto wa shule, lenye namba za usajili T 279 AQN, lililokuwa likitokea maeneo ya mjini likielekea pande za Njiro na vitongoji vyake, kwa ajili ya kuwakusanya wanafunzi kwenye majumba yao na kuwapeleka shuleni. Katika tukio hili, hakuna mtu yeyote yule aliyejeruhiwa wala kuumia; ila magari, na hasa dogo la rangi nyeupe, ndiyo yaliyoumia vibaya.
No comments:
Post a Comment