NDIYO MAANA SIKU ZOTE MIMI HUWA NASEMA: "JAMANI, UTOTO RAHA!"
Wakwetu, hivi karibuni Mpini Wa Shoka ulikuwa umehudhuria kwenye shughuli ya dua ya marehemu kwenye familia moja maeneo ya M'bauda-Arusha (barabara ya Arusha-Simanjiro-Kiteto). Sasa wakati shughuli hiyo ikiendelea, ndipo nikagundua kikundi cha watoto hawa ambao baadhi yao wananihusu mimi, wao walikuwa wamezama kwenye pilikapilika zao nyingine kabisa. Walikuwa wamezama kwenye michezo yao kama unavyowaona kwenye picha hizi. Sasa hebu angalia mwenyewe jinsi kila mmoja alivyo na mtindo wake binafsi wa kucheza! Wengine kama vile wamelala usingizi, kumbe wapi, wakwetu! Wako macho! Ni michezo tu!
No comments:
Post a Comment