MSIBA HALMASHAURI YA WILAYA YA ARUSHA (ARUSHA VIJIJINI)

Siku ya Ijumaa ya tarehe 10/05/2013, maofisa na watumishi wa idara mbalimbali katika Halmashauri ya  wilaya ya Arusha (Arusha Vijijini) walijikuta katika majonzi baada ya kumpoteza mmoja wa maofisa wake Bw. Liberatus Lokisa, ambaye alikuwa ni Ofisa Mtaalamu wa mfumo wa umwagiliaji. Marehemu Liberatus alifia katika hospitali ya A.I.C.C jijini Arusha, na mwili wake ukasafirishwa kwa ajili ya mazishi siku ya Jumatatu ya tarehe 14/05/2013 kwenda nyumbani kwao eneo la Olele-Rombo Mashati-mkoani Kilimanjaro. Marehemu alikuwa akiishi eneo la Mianzini, Arusha; na ameacha watoto watatu na wajukuu wawili. Mpini Wa Shoka ulihudhuria katika shughuli ya maziko eneo la Olele-Rombo Mashati....




Baadhi ya vyombo vya moto vilivyousafirisha mwili wa marehemu Liberatus Lokisa kutoka jijini Arusha hadi katika eneo hili la Olele-Rombo Mashati-mkoani Kilimanjaro




Sehemu ya umati wa waombolezaji, wake kwa waume, wenyeji kwa wageni...




Wazee wa familia nao walikuwepo...




Vijana wakishughulika kulitayarisha kaburi...




Pembeni ya kaburi lililochimbwa likiusubiri mwili wa marehemu Liberatus Lokisa tayari kwa maziko, panaonekana kaburi jingine lenye majani kwa juu. Hili ni kaburi la mke wa marehemu Liberatus Lokisa, marehemu Marry Truai, aliyefariki mwaka 1995; ambapo walibahatika kupata watoto watatu: Kelvin, Margreth na Signi.




Sanduku lenye mwili wa marehemu Liberatus Lokisa likiteremshwa kaburini..




Tayari sanduku limekwishalazwa kaburini




Kazi ya kulifukia kaburi ikachukua nafasi





Kisha uwekaji wa maua na mashada kwa makundi mbalimbali juu ya kaburi ukafuata




Watoto wa marehemu: Kelvin, Margreth na Signi (waliosimama katikati) wakishuhudia kwa uchungu na tafakari nyingi hatua zote za maziko ya baba yao mpendwa, marehemu Liberatus Lokisa.




Maofisa na watumishi wa idara mbalimbali katika Halmashauri ya wilaya ya Arusha (Arusha Vijijini) walihudhuria kwa wingi katika shughuli ya kumhifadhi mtumishi mwenzao. Hawa ni baadhi tu ya maofisa na watumishi hao. Aliyeko mbele kabisa ya picha (mwenye suti nyeusi) ni Ofisa umwagiliaji wa Halmashauri ya  wilaya ya Arusha (Arusha Vijijini) Bw. Paulus Kessy ambaye ndiye aliyemwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Arusha (Arusha Vijijini). Na mwenye miwani nyuma ya Bwana Kessy ni Bwana Dixon Andindilile, mhasibu (Bwana fedha) wa TASAF wilaya ya Arusha (Arusha Vijijini)

"Kwa hakika, ukitaka kuudhibiti moyo wa chuki, hasira na husuda, basi wakati wote kikumbuke kifo japo kidogo tu!"




No comments: