NI VIGEREGERE, NDEREMO NA VIFIJO; BIBI KAPATA BWANA, BWANA KAPATA BIBI! KAMA WEWE UNA WIVU, UTAJIJUA MWENYEWE....!
Ilikuwa ni Siku mpya kabisa katika maisha yao. Siku itakayobaki daima ndani ya kumbukumbu zao. Siku ya Jumamosi ya tarehe 18/05/2013, kwenye ukumbi wa El Nois uliopo eneo la Kwa Iddi-Arusha (barabara ya Arusha-Namanga-Nairobi), ambapo Bw. Theophile 'Teo' Leonard, Ofisa Wizara ya Maliasili na Utalii-Kibaha, Pwani alipouaga rasmi ukapera kwa kufunga ndoa na Bi. Bahati Mtweve, Ofisa Biashara wa wilaya katika halmashauri yaWilaya Arusha (Arusha Vijijini)...
Mpini Wa Shoka nao ulikuwemo ndani ya ukumbi wa El Nois....
Wakiwa katika pozi rasmi la Mke na Mume
Bibi na Bwana Harusi kila mmojawao akafanya mbwembwe zake za kuwasha mshumaa kwenye keki...
Bw. Theophile 'Teo' Leonard akiwa ameibeba mojawapo ya keki zilizoandaliwa kwa ajili ya kutolewa zawadi, huku Bi harusi, Bahati Mtweve, akiwa katika tabasamu la nguvu
MC, (msema chochote....mwongozaji wa shughuli). Bw. Otuman Alex Mahundi, ndani ya mavazi ya kiasili, akiwa kazini kwa kasi na ari kubwa
Bwana na Bibi Harusi mbele ya ndafu; kisu mikononi wakiwa wamekiinua juu kwa pamoja tayari kabisa kwa ajili ya kukizindua rasmi kitoweo hiki kilichopo mbele yao...
Sehemu ya ndugu, jamaa, majirani, marafiki na watumishi kutoka pande mbalimbali za Mji wa Arusha na mikoa mingine nchini Tanzania waliohudhuria, wakiwa katika meza zao wakiifuatilia shughuli kwa umakini wote
Kaka mlezi wa Bwana Harusi, Injinia Revocatus 'Revo' Mwankemwa wa kampuni ya Helios Towers ya jijini Arusha akiwa katika pozi la furaha ndani ya ukumbi pamoja na mkewe, Bi. Lydia Moshi
Baba na mama wa Bwana Harusi
Baba na mama wa Bibi Harusi (Mr & Mrs Mtweve).
(Samahani kwa kamera kuteleza kidogo)
Zawadi za maharusi kutoka kwa waliohudhuria.....
Kwenye shughuli kama hizi, vituko na vibweka huwa havikosekani! Tangu Mpini Wa Shoka ulipotumbukia ndani ya ukumbi huu, uliona na kukutana na vituko chungu nzima. Lakini hiki kiliniacha na maswali kadhaa kichwani. Hebu nikushirikishe na weye. Eti, hivi hiki ndio kivazi cha aina gani! Huyu kajifunika kweli mwili, au yuko wazi tu kama huyo mwenziwe pembeni kushoto! Na hiki alichojifunika ni kitu gani hasa! Ni nailoni, au!
Miserebuko ya kila aina, hasa ile ya ngoma za kiasili, nayo haikukosekana...
Hao! Hao! Wakina dada na miondoko yao ya kuzunguruka..
Wanakamati (wasimamizi na waandaji wa shughuli hii nzima, nje na ndani ya ukumbi) nao hawakuwa nyuma. Hapa wakiwa wamejimwaga kwa pamoja na suti zao wakiserebuka vilivyo...
Picha za kumbukumbu nazo hazikusahaulika kamwe...
Bibi Harusi na Bwana Harusi wakiwa katika picha ya pamoja na familia ya upande wa Bwana Harusi
Picha ya pamoja na familia ya upande wa Bibi Harusi
Baadhi ya watumishi wenziwe na Bibi Harusi katika halmashauri ya Wilaya ya Arusha (Arusha Vijijini), nao hawakujivunga kupata picha ya pamoja na mtumishi mwenzao...
2 comments:
Anonymous
said...
asante kwa picha na habri napenda sana blog yako big it up
2 comments:
asante kwa picha na habri napenda sana blog yako big it up
eee nimeipenda hiyo.katika tembelea tembelea yangu nikashangaa kukutana na blog yenye picha zangu za harusi...kazi nzuri,,,its me bi harusi bahati
Post a Comment