URAFIKI, UDUGU NA UJAMAA USIWE WAKATI TUNAPOKUWA HAI TU TUKIPUMUA! TUKUMBUKANE HATA WAKATI TUNAPOKUWA TUMETENGANISHWA KWA KIFO.


Mpini Wa Shoka uliwanasa wanafamilia hawa wakiwa ndani ya eneo la makaburi katika Mji wa Ngaramtoni ya Chini-jijini Arusha, wakiwa katika harakati za kulifanyia usafi wa kuling'olea majani kaburi la mmoja wa wanafamilia wao aliyefariki miezi kadhaa iliyopita. Ni vema kuuendeleza Urafiki, Ujamaa na Udugu wetu kama hivi kwa wale tuliokuwa tukiwapenda, japo wao tayari hawapo tena pamoja nasi katika uhai wa dunia hii. Tusisahau pia kuwaombea na dua njema kwa Mwenyezi Mungu aliyetuumba sisi na wao waliokwishatangulia. Dunia mapito jama! 

No comments: