MPINI WA SHOKA NDANI YA MARANGU-SAMANGA; KILIMANJARO.


Sehemu ya daladala tulizotoka nazo jijini Arusha hadi Marangu...




Daladala za Marangu zikichuana (ushindani) kwenye mpando mkali. Ndani yake mna abiria wa kutosha!




Jionee mwenyewe utamu wa lami. Hii ni barabara iliyopo kwenye mteremko mkali sana; Marangu hadi Mwika. Madereva hawaujali ukali wa mteremko huu! Hapa vyombo vya moto vinakimbizwa kwa kasi ya kutosha kama Mpini Wa Shoka ulivyoshuhudia!





Baadhi ya nyumba na uzio wa kuvutia wa maua uliopambwa kwa mazao kadhaa na hasa migomba; Marangu-Samanga




Shughuli za biashara kama hivi unavyojionea nazo pia zipo kwa wingi...




Unayaona haya mazao ambayo tayari yamekwishavunwa yakisubiri kuwaendea wanunuzi; yawezekana wanunuzi hao ni mimi au wewe. Ndizi za Marangu-Samanga.




NYUMBA ZA IBADA NAZO PIA ZIPO....

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Marangu-Samanga.



 

Msikiti, Marangu-Samanga.


No comments: