MSIBA; MARANGU-KILIMANJARO
Hivi karibuni Mpini
Wa Shoka ulisafiri hadi Marangu mkoani
Kilimanjaro; Kaskazini mwa Tanzania
na kushiriki safari ya mwisho hapa
duniani (mazishi) ya mpendwa wetu, rafiki yetu, ndugu yetu, dada yetu, mama
yetu Caides Mature aliyefariki siku ya Jumatatu tarehe 22/04/2013 katika
hospitali ya Seliani jijini Arusha. Mwili wa marehemu ulisafirishwa kutoka
hospitali ya Seliani kwenda Marangu-kwa mazishi siku ya Jumamosi tarehe
27/04/2013 na kuzikwa siku hiyohiyo nyumbani kwao Marangu-Samanga (ujombani-kwa
ukoo wa Mawalla). Ameacha familia ya watoto kadhaa. Poleni sana ukoo wa Mawalla (ujombani) pamoja na ukoo wa Mosha (upande wa baba.)
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa karibu
wakiwa wamevalia fulana zenye picha ya marehemu Caides Mature.
Makundi ya watu kutoka pande mbalimbali za
Tanzania na hata nje ya nchi, yakiwasili eneo la msiba, Marangu-Samanga.
Wale waliowahi kufika wakiwa tayari wamejituliza
kwenye viti wakiifuatilia ratiba ya mazishi.
Ama, Kwa hakika, sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu, na
sote kwake tutarejea tu, kwa maana hiyo ni ahadi yake thabiti isiyoweza kamwe
kubadilishwa wala kugeuzwa na yeyote yule kwamba, kila nafsi(kila chenye uhai)
ni lazima kitayaonja mauti.
Basi na wewe unapofanikiwa kuyahudhuria mazishi ya mwenzio kama hivi, ni fursa nzuri ya kuihoji nafsi yako, "je wakati na wewe utakapofikwa na umauti na kufanyiwa shughuli kama hii, nafasi yako mbele ya yule aliyekuumba unayekwenda kwake ni ipi? Maisha yako ya kila siku hapa duniani yanayo heri yoyote ile itakayokufanya uwe salama mbele zake?" Anza sasa kujitathmini.
No comments:
Post a Comment