AJALI KALI..! ASKARI WA USALAMA WA BARABARANI MKO WAPI MPIME HAPA!


Kwenye kona hii iliyopo ubavuni mwa Ofisi ya kununulia na kuuzia chuma chakavu (TransCrap) katika mtaa wa Jamhuri (Jaluo Street)-Arusha Town, Mpini Wa Shoka ulilifumania live tukio hili la bwana mdogo huyu, ambaye alijikuta akipiga mweleka wa aina yake, baada ya baiskeli hii aliyokuwa akiiendesha kwa kasi kumshinda maarifa na kumbwaga chini jirani kabisa na chemba ya maji machafu...



Anainyanyua baiskeli baada ya ajali...



Anaiweka sawa tayari kwa kuondoka, baada ya kuhakikisha kwamba yeye pamoja baiskeli yake wote wawili hawakuumia wala kujeruhiwa popote pale...


No comments: