BARABARA YA AFRIKA MASHARIKI; ARUSHA-NAMANGA-NAIROBI...


Yawezekana una miaka mingi sana haujafika katika Jiji la Arusha. Au upo ndani ya Jiji hili, lakini kwa muda mrefu haujabahatika kabisa kupita katika barabara hii. Kwa sehemu kubwa imekwishakamilika. Na hata mataa ya barabarani yamekwishawekwa kama ambavyo nguzo zake zinavyoonekana vema kwenye picha hii. Hapa ni eneo la OilCom-Sakina, jirani kabisa na eneo la Kwa Iddi (Kona ya kwa Lowasa). Wakati huu ni wa Asubuhi ya Saa mbili; magari yanakwenda kasi kwelikweli. Ni utamu kunoga kwa madereva, lakini ni hatari tupu, Wakwetu! 


No comments: