HATA KAMA WEWE NI JASIRI KWA KIASI GANI, LAKINI MBELE YA USINGIZI, Wakwetu, HAUFURUKUTI! UKIKUITA NI LAZIMA UTAITIKA TU! NA UKIJIFANYA UNAJITAHIDI KUGOMA, BASI UJUE KABISA KWAMBA MAHALI POPOTE PALE UTAKAPOJIEGESHA, hata kama ni ofisini, NI LAZIMA 'utakunyakua tu' KAMA HIVI!

Fundi maarufu wa pikipiki mjini Arusha, Fundi Abdallah akiwa 'ameutwanga' vilivyo usingizi akiwa amejiegemeza ukutani kwenye kijiwe (ofisi) chake cha kazi. Yawezekana baada ya kuwasubiri wateja kwa muda mrefu bila ya mafanikio, ndipo akaamua ajipumzishe kidogo kwa mtindo huu! Ni mwendo wa majira ya kama saa 7 hivi za mchana. Anayeonekana pembeni yake ni fundi wa baiskeli, Fundi Samoraa.

No comments: