HAPA SIJAJUA KAMA NAPO PIA Wachina WANAJIANDAA KUTAKA KUANZA KUPAFANYIA Vitu VYAO, AU VIPI!
Ni kwenye Mtaa wa Jamhuri Kata ya Daraja Mbili. Vifusi vya kokoto laini vikisubiri kusambazwa. Kazi ya 'kulilambisha' lami Jiji la Arusha inazidi kupambana moto, kama ambavyo mara kadhaa Mpini Wa Shoka umekuwa ukikutupia mbili 3 hapa na pale. Lakini kama eneo hili la Daraja Mbili nalo pia limo katika orodha ya barabara zake kutaka 'kulambishwa' lami, basi ni wazi majengo yake mengi ya wakazi na wenyeji wa hapa itabidi yakubali tu 'kusalimu amri' na kubomolewa, kwa jinsi yalivyozisogelea mno barabara...! Kweli, Ukiutaka uzuri, basi ni sharti ukubali kudhurika! Kazi ipo, mwanakwetu!
No comments:
Post a Comment