ACHA MASIHARA, WEWE! UKISIKIA KAZI NI KAZI KWA JINSIA ZOTE, BASI HIVI NDIVYO Mpini Wa Shoka ULIVYOINASA ACTION HII Live BILA YA CHENGA!
....ni majira ya saa 6 za mchana hivi, siku ya Jumatatu, wakati Mpini Wa shoka ulipokuwa ukikatiza kwenye mitaa kadhaa ya Jiji la Arusha, mara ghafla mbele yake ukakutana na tukio hili la wakina mama hawa wawili waliokuwa wakifanya kazi ambayo, hata baadhi ya wanaume waliokuwa wakiwatazama kwa pembeni walibaki wakiwashangaa tu kwa jinsi walivyokuwa wakijituma kwa bidii....! Mmoja alikuwa juu ya gari aina ya Fusso akibeba matofali na kuyapanga vema ndani ya gari hili; na mwenzake akiwa chini na sululu yake mkononi aking'oa na kuyabomoa matofali yaliyokamatana na nondo za renta kwenye ukuta uliobomolewa kwenye kituo cha kuoshea magari (Jamhuri carwash), kilichopo kwenye mtaa wa Jamhuri (Jaluo Street) katika Kata ya Daraja Mbili.
Hapa hakuna kuremba; ni kazi tu...
Aliyeko chini ilimbidi mara kadhaa aitupe pembeni sululu, na kuamua kuitumia mikono yake ili kujaribu kuyapangua matofali na kumpatia mwenziwe aliyeko juu ya gari. Sasa ndugu yangu, kama mmoja wa hawa wakinamama ni mkeo, basi Mpini Wa Shoka unakushauri ujichunge sana. Kwani, siku utakayojaribu kumletea ukorofi unaweza ukajikuta ndani ya matata na matatizo makubwa; na hata huenda ukajikuta ukichezea kichapo (kipigo) cha maana. Wewe mwenyewe si unaona jinsi wanavyopiga kazi hapa bila ya wasiwasi wowote ule!
No comments:
Post a Comment