SIKU ZA JUMAPILI; SOKO KUU-ARUSHA
Hivi ndivyo hali ya mambo huwa katika siku za Jumapili, kwenye barabara zote zinazolizunguka eneo la Soko Kuu jijini Arusha. Barabara zote wakati mwingine huzibwa kabisa na wafanyabiashara hawa wa kila aina, wazee kwa vijana-wake kwa waume. Kwa siku za kawaida, yaani J'3, J'4, J'5, Alhamisi Ijumaa na hata wakati mwingine hadi J'mosi, huwa ni marufuku kabisa kwa mfanyabiashara yeyote yule kuonekana akifanya biashara yake katika maeneo ya barabara hizi; na huwa wanakuwepo askari (mgambo) wa halmashauri ya Jiji, ambao hufanya doria kali ili kuwadhibiti na kuwakamata wafanyabiashara hawa. Wengi wa wafanyabiashara hawa ni wale waliopewa hivi karibuni eneo jipya la kufanyia biashara zao katika uwanja mkubwa wa N.M.C uliopo jirani tu na Soko hili Kuu la Arusha. Sasa kwa siku za Jumapili, ambazo huwa hakuna ulinzi wala zuio la aina yoyote ile, ndipo na wao huamua kujimwaga kwa raha zao kwenye barabara zote za Soko hili Kuu kama unavyojionea mwenyewe, kiasi ambacho huwa ni kazi ngumu kwa wale wenye vyombo vya moto (usafiri) wanaotaka kuzitumia barabara hizi. Na hasa mahali pa kuegesha magari ndipo huwa ni kazi ngumu kwelikweli.
Sehemu ya wafanyabiashara hao na bidhaa zao. Chagua; bei ni poooooooa! Ushindwe tu mwenyewe kuvaa na kupendeza....
Zamani ilikuwa ni vigumu mno kuziona baadhi ya bidhaa zikiuzwa kwa uwazi mkubwa kama huu, na hasa zile za wakinamama. Zilikuwa zinaonekana kuleta 'ukakasi' na aibu nyingi machoni. Lakini siku hizi hakuna tena mambo ya kuoneana aibu. Ni biashara tu kwa kwenda mbele! Hizi ni bidhaa muhimu kwa wakina mama. Ni bidhaa za mtumba. Hapa, Wakwetu, wakina mama wanajichagulia chochote wakipendacho bila ya 'presha' wala woga wowote ule! Hapa zipo Sidiria..! Magaguro..! Vyupi (underwear) vya kila aina na kila saiz (Size); hata zile za over saiz ya mwisho kabisa yawezekana nazo pia zinapatikana hapa! Na bei hapa, Wakwetu, ni karibu na dezo (bure) kabisa. Ni kuanzia Tshs elfu 1, elfu 2, elfu 3 hadi elfu 4! Hayo ni mambo ya kila siku za Jumapili, kwenye barabara zinazolizunguka Soko Kuu la Jiji la Arusha. Na wewe mwanamama, vipi! Lini utakuja kuchagua saiz yako hapa! Na hata wewe mwanababa, unaonaje ukafika hapa One Sunday ukamchagulia U're lovely .... naniii za kutosha kabisa kwa bei poa! Acha woga wewe; njoo tu; Mpini Wa Shoka hautokupiga picha.
No comments:
Post a Comment