Leo ndio mechi za Robo fainali ya michuano ya kandanda ya kombe la chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki. Na mechi kali kabisa ni kati ya Tanzania Bara 'The Kilimanjaro Stars' dhidi ya Uganda 'The Cranes'. Michuano inayofanyika nchini Kenya. Lakini katika pitapita za Mpini Wa Shoka huku na kule, nimeshuhudia mabango ya matangazo mitaani siyo mengi sana yanayozitangaza mechi za michuano hii! Sielewi ni kwa nini! Lakini hamasa kubwa wakati wote ni katika ligi kuu ya kandanda ya nchini Uingereza. Mfano mzuri ni kama bango hili la mechi zilizopita jinsi lilivyoandikwa kwa mbwembwe na umaridadi mkubwa, japo matokeo ya mechi ya Man U iliwasononesha mno mashabiki wake, baada ya 'kubonyezwa' na Everton, huku Arsenal 'ikifanya kweli' mbele ya Hully City...


No comments: