Tiba zingine, bwana!! Hebu shangaa hata wewe! Jamaa mwenye fulana nyeupe anaitwa Felichismi Fidelis Tarimo "baba Sharon", maarufu zaidi kwa jina la 'Felii'. Mpini Wa Shoka ulimfuma mtaa wa Jamhuri-Arusha City akipewa dozi ya mmea wa Alovera 'shubiri' na huyu ndugu aliyekuwa akiitembeza mitaani tiba hii. Sasa sikuelewa Felii alikuwa ni mgonjwa! Au alikuwa anaonja ladha ya mmea huu jinsi ilivyo tamu! Lakini hapa kipimo sahihi cha hii dozi ni kipi hasa! Labda ni makadirio tu ya macho ya muuzaji....!


Kaka, hivi eti alovera 'shubiri' huwa ni chungu au ni tamu...!




Hebu ngoja nionje mwenyewe nijue...




  Mmmmh! Wewe! Mbona ni chungu namna hii! Hii inatibu kitu gani hasa mwilini, maana najihisi kama vile roho inataka kunichomoka! hatari!

No comments: