Jioni ya Jumapili ya tarehe 01/12/2013, Familia ya Bwana Gilbart Erasto Massawe ya Sanawari ya Juu Arusha, waliungana pamoja katika sherehe ya kumpongeza mtoto wao, Elly Erasto Massawe kwa kupata kipaimara. Sherehe hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa shule ya Green Acres-Sekei Arusha....


Kushoto ndiye mtoto aliyekuwa akipongezwa, Elly. Kulia ni mpambe wake, Godi J. Mshanga; wakipata mlo. 




Bwana na Bibi Gilbart Erasto Massawe wakiwa katika pozi wakati sherehe zikiendelea ukumbini 

 


 

Idadi ya waliohudhuria, ndugu, jamaa na marafiki kutoka pande mbalimbali, ilikuwa ni kubwa....




Mambo ya 'kujichana' yalikuwepo ya kutosha kabisa....





Mezani kwa wanafamilia napo palisheheni




KWA KAWAIDA SHUGHULI KAMA HIZI ZA WATOTO, WAZEE NDIO MAHALI PAKE ILI KUWAPA NGUVU WAJUKUU ZAO!






USIONE HAYA! PIGA VITU.

Mwendo mdundo; jicho na sahani, sahani na jicho!

Wakati wa 'kumenya vitu' kazi ilikuwa ni moja tu, wakubwa kwa wadogo, wazee kwa vijana, wake kwa waume




Hata wenye watoto wadogo hawakuwaacha nyumbani. 'Waliwabandika' viunoni...




 Wakati wa zawadi na kupongezwa...

Hongera sana kijana...





Hawa wenyewe walikuwa nje kabisa ya ukumbi; tena ni kwenye giza. Nikawafuma 'wakiserebuka' vilivyo! Hatari...!

No comments: