HAPA NI KATIKA MOJAWAPO YA VIJIJI WILAYANI KARAGWE MKOANI KAGERA. MY WAIFU (wife) ALIKUWA HUKO KWA ZIARA YA KIKAZI. AKAPATA PICHA MBILI TATU HAPA! NAJUA UNAWAZA KWA HARAKA ENDAPO MOTO UKIIBUKA NA WEWE UKIWA UMELALA NDANI YA NYUMBA HII INAKUWAJE! LAKINI MBONA HATA NYUMBA ZILIZOJENGWA KWA MATOFALI NAZO PIA HUWA ZINAUNGUA TU NA KUTEKETEA KABISA. ACHANA NA WASIWASI HUO. SWALI LANGU KWAKO NI HILI: KWA MFANO WEWE NA FAMILIA YAKO HII NDIO NYUMBA YENU, NA IPO JIRANI KABISA NA MSITU WA HIFADHI YA WANYAMAPORI, JE, BWANA MKUBWA NDOVU AMA NDUGUYE FARU 'WAKICHAFUKWA' (Wakikasirika) NA KUAMUA KUELEKEA PANDE ZA NYUMBANI KWAKO, WEWE NA FAMILIA YAKO MTAJIBANZA KWENYE UPANDE UPI HASA WA UKUTA AMBAO NI IMARA ZAIDI KWENYE NYUMBA HII?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment