WAKWETU, SOMA MWENYEWE UONE!


Tarehe 10/12/2013, mwendo wa saa mbili ya usiku, nilikuwa nimejipumzisha chumbani baada kurejea kutoka kwenye kazi za mchana kutwa nje kidogo ya Mji wa Mtwara, nikafungulia mojawapo ya kituo kikubwa cha Televisheni nchini Tanzania ili kuangalia taarifa ya habari, na hasa katika kipindi hiki cha maombolezo ya kifo cha Mzee Nelson Mandela. Tangu taarifa ya habari ilipoanza kurushwa katika kituo hiki cha Televisheni, maelezo haya yenye makosa yalikuwa yakipita muda wote. Nilidhani mhariri wa kituo, au hata watumishi wengine wangeweza kushituka na kufanya maarifa ya marekebisho kwa haraka, lakini hadi taarifa hiyo ya habari ilipotia nanga mwendo wa saa tatu ya usiku na kuipisha Taarifa ya habari ya Kiswahili kutoka shirika la Uingereza-BBC, makosa hayo hayakubadilishwa kamwe! Mpini Wa Shoka ukajiuliza sana endapo wenye televisheni hii huwa wanaturushia habari sisi wananchi, lakini yawezekana wao wenyewe huwa hawaangalii (hawatazami) kabisa televisheni yao! Yawezekana....


Makosa hayo ni neno 'VIONGO' badala ya Viongozi, pamoja na 'MABALIMBALI' badala ya Mbalimbali.

No comments: