Tangu J'3 ya tarehe 09/12/2013 hadi Ijumaa ya tarehe 13/12/2013, nilikuwa hapa kwenye kituo kipya cha Redio ya jamii kwa ajili ya kuwapa ushirikiano wa kimafunzo, na hasa katika 'uwanja' wa uandaaji, utengenezaji na urushaji wa vipindi. Wako mbioni kituo kufunguliwa na kuanza kurusha matangazo wakati wowote kuanzia mapema mwaka 2014. Kituo hiki cha Redio ya jamii (Jamii FM), kipo nje kidogo ya Mji wa Mtwara, kwenye Kijiji cha Naliendele. Jirani kabisa na eneo la uwanja wa kumbukumbu ya mashujaa wa mapambano ya vita vya kusini mwa Afrika; mwendo wa kama Km 12 hivi, kwenye barabara Kuu ya Mtwara-Newala, kupitia Tandahimba....


Karibu sana...




Shaffii Ndege(kushoto) na Mohamed Massanga; miongoni mwa vijana wa kituo hiki.... 




hebu jaribu kulibeba niuone uwezo wako! Anaitwa Amua Rushita; Mtayarishaji wa vipindi pamoja na mtaalamu wa mitambo na kompyuta



 

Chumba cha kutayarishia habari (news room)





Vijana wakiwa makini pamoja na mwezeshaji wa mafunzo haya kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bi. Sylvia Mwehozi (katikati), wakati wa mojawapo ya kazi za vitendo ndani ya chumba cha kutayarishia vipindi (production studio)





Mojawapo ya picha maridadi za kuvutia siku ya mwisho ya mafunzo. Kwa picha ya chini: waliosimama (kutoka kushoto) ni Juma Chikambu, Bi. Sylvia Mwehozi (mwezeshaji wa mafunzo), Swetbert Chilamula, Shaffii Ndege, Fakihi Mussa (mmoja wa viongozi na waanzilishi wa kituo hiki), Christopher Mpambichile (dereva) na Amua Rushita.  

Waliochuchuma (kutoka kulia ni Patricia Nchia, Gregory Millanzi mohamed Massanga. Ni MpiniWa Shoka pekee ndio hauonekani hapa, kwa sababu ndio uliokuwa ukikuchukulia picha hizi. Kama vipi, geuza picha kwa nyuma utauona...





Acha kabisa! Pozi la nguvu.... pozi la kukata na kucha! Patricia Nchia, Gregory Millanzi na Swetbert Chilamula...

No comments: