Kila kazi inahitaji maarifa, ufundi na ujuzi unaostahili, ndipo itapata heshima na kukubalika ipasavyo... Usipokuwa na maarifa, ufundi na ujuzi unaostahili, wakwetu angalia usije ukaumbuka...


Jicho la Mpini Wa Shoka lilimnasa Mama Hawa Ramadhani maarufu kwa jina la mama Fatuma wa mtaa wa Jamhuri (Jaluo Street) jijini Arusha, akiwa 'mitamboni' akikaanga vitumbua kwa ajili ya wateja wake. Wateja wanaposifia bidhaa, basi ujue utaalamu wa mtengenezaji ndio unaostahili sifa hizo. Hata vitumbua vikisifiwa kwa utamu na uzuri wake, basi ujue mtayayarishaji na mpishi wa vitumbua hivyo ndiye anayestahili sifa hizo...

No comments: