...Kwa hakika, Mpini Wa Shoka unatoa pole ya kutosha kwa wale wote mliokumbwa na zoezi la bomoabomoa ya jijini Arusha. Ama kweli, Mpini Wa Shoka umeamini kwamba "kufa kufaana!" Wakati waliokuwa wakivunjiwa nyumba zao walikuwa katika hekaheka za kujiokolea hiki au kile; majirani na hata wa mitaa ya mbali waliofika katika maeneo ya matukio hayo, Kilombero, Themi "faya" na Kaloleni, wao waligeuka wanyakuzi wa hatari! Aisee, ilikuwa ni hatari isiyofaa hata kuielezea! Ama kweli, kwenye haya maisha iko kazi, wakwetu! Lakini pia ni vema wananchi tukajifunza; hasa juu ya zoezi lolote lile linaloitwa ni la Serikali! Anza kuangalia ustaarabu wako mapema, kabla haujaadhirika....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment