AMA KWELI, MAISHA NI KITU KINGINE! PAMBANA TU, WALA MTU YEYOTE YULE ASIKUKATISHE TAMAA. IKO SIKU 'utatoboa' TU!
Yawezekana kabisa ni mmojawapo wa wapiga picha maarufu na wakongwe ndani ya vitongoji na mitaa ya jiji la Arusha. Ni miaka mingi sana tangu nilipoanza kumfahamu. Alikuwa ni mpiga picha wa kawaida tu. Na baada ya mapambano ya miaka chungu tele, leo jamaa amepiga hatua mpya! Siku hizi anamiliki ofisi yake ndogo ya masuala ya picha! Huduma ya Paspotsize pamoja na aina zote za picha zinapatikana hapa. Na mpigaji ni yeye mwenyewe! Anaitwa bwana Twaha Husseni.
Tabasamu la nguvu mbele ya jicho la Mpini wa Shoka ndani ya ofisi yake.
Ofisi hii ipo mtaa wa Ndovu; jiranijirani kbs na jengo la CCM-Mkoa wa Arusha na uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid. Hongera sana swahiba.
No comments:
Post a Comment