SOKO LA KILA SIKU YA JUMAPILI-MONDULI MJINI...


Ndani ya J'pili moja, katika pitapita zake, Mpini Wa Shoka ukajikuta umetua katika Mji wa Monduli (wastani wa kama km 34 au pungufu kidogo tu kutoka Arusha town). Nikafika kwenye soko hili (gulio) ambalo hufanyika mara moja tu kwa wiki (siku ya Jumapili pekee). Hapa zinauzwa bidhaa mbalimbali, lakini zaidi ni mazao na mifugo.... 

Sagulasagula; wateja na wauzaji wakiwa wamechanganyika vilivyo...





Mambo ya 'msosi' nayo ni kama kawaida. Mwenyewe si unajionea....




Ndondo (Maharagwe) la njano-Soya





Ndondo (Maharagwe) jekundu





Bidhaa nyingine zinateremshwa na nyingine zinapakizwa kwenye vyombo vya usafiri, na kusafirishwa maeneo mbalimbali...





Tatizo linaloonekana wazi ni kwamba, soko hili linahitaji kuboreshwa mno. Hebu fikiria, endapo mvua ya maana 'ikiteremka' vilivyo, hapa panafaa hata kutembea tu, achilia mbali kuuza bidhaa? Hii ni mojawapo ya barabara zinazolizunguka soko hili... Na wewe ukipata nafasi, basi Jumapili moja fika hapa ujinunulie 'msosi' kutoka kwa wakulima na wafugaji wa Monduli upeleke home.

No comments: