Lahaula! NDANI YA MTARO! Miguu juu!


Hili huenda lilikuwa ni mojawapo ya matukio ya kuuaga mwezi wa Kwanza 2014, na kuukaribisha mwezi wa Pili 2014! Mpini Wa Shoka ulilishuhudia basi hili la kiwanda cha nguo cha SunFlag kilichopo Jijini Arusha likiwa limetumbukia mtaroni pembezoni kidogo mwa geti la Ofisi za maafande wa Kikosi cha Zimamoto (fire rescue) wa Arusha, jirani na eneo la Sinoni. Lilikuwa likitokea Njiro, na lilikuwa limesheni wafanyakazi tele ndani yake (wa kike kwa wa kiume)... Hakuna aliyekufa. Waliumiaumia tu hapa na pale, na baadhi yao kukimbizwa hospitali Kuu ya Mkoa wa Arusha (Mount Meru)... 


Ni kwenye mzunguko(keepleft) kipya cha faya (fire), dereva alimwagika nalo; likamshinda maarifa... mbio za sakafuni!









Kama kawaida, wa kushangaashangaa nao huwa hatukosekani (wakubwa kwa wadogo). Kila mmoja hapa anatoa ushuhuda na maelezo yake....

No comments: