Kijiji Cha Naliendele; Mwendo wa kilometa 12 tu kutoka katikati ya Mji wa Mtwara. Hapa ndipo siku siyo nyingi sana kituo kipya cha redio ya Jamii (Jamii Fm-Mtwara) kitaanza kurusha matangazo yake...
Japo ni kijijini, lakini mandhari ya eneo hili ni ya kuvutia sana...
...hapa kila upande ni miti ya miembe na minazi mitupu! Yaani ni matunda tu kwa kwenda mbele! Embe dodo kubwa kabisa unalolijua wewe katika eneo lako, hapa linaanzia bei ya Tshs 100/- hadi 150/- tu! Afya itaacha kuja yenyewe, wakwetu? Hapa hapahitajiki hadi daktari akupe ushauri. Ni kujilia matunda tu kila dakika kwa kwenda mbele.
Baadhi ya mitaa na vichochoro vya sehemu tu ya kijiji cha Naliendele. Hapa ni jirani kabisa na kilipo kituo cha redio mpya ya 'Jamii FM'. Uzio wa kituo cha redio mkono wa kulia... Wakwetu, kuzunguka na kutembelea maeneo mbalimbali tofauti, nayo pia ni elimu na maarifa makubwa. Siyo kung'ang'ania tu sehemu moja kila siku kama jiwe la kuanikia unga kijijini...
No comments:
Post a Comment