Wanahabari wa Mtwara ndani ya Semina ya Siku 1. Semina iliyofanyika kwenye ukumbi wa Bodi ya Korosho, Mtwara Mjini siku ya Jumanne-17/12/2013. Semina iliandaliwa na kuratibiwa na Shirika la Habari na mawasiliano la MtuKwao-Mtwara. Wawakilishi wa Mashirika kadhaa yasiyokuwa ya kiserikali 'N.G.O's', viongozi wa serikali Mkoa wa Mtwara katika ngazi mbalimbali nao pia walikuwepo ...Mpini Wa Shoka nao ulihudhuria...

Wanahabari wakiwa makini wakifuatilia semina kwa utulivu...





Mwandishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania-TBC, kituo cha Mtwara, Peter Makorongo (aliyekaa katikati) naye pia alikuwepo. Mwenye miwani kushoto ni Christopher Mpambichile wa shirika la habari la MtuKwao-Mtwara.





Sehemu ya mafunzo ya kubadilishana mawazo... yalikuwa matamu mno yaliyohitaji hata muda wa wiki nzima.





Mwenyekiti wa wanahabari wa Mkoa wa Mtwara (Mtwara press), Hassan Simba, (aliyekaa kwa nyuma) naye pia alikuwepo.  Hapa anaonekana akichangia jambo...





Bwana Swallah Saidi Swallah, Mkurugenzi Shirika la Habari na mawasiliano la MtuKwao-Mtwara ambalo liko mbioni kuanza matangazo ya kituo chake kipya cha Redio, "Jamii FM",  ndiye aliyekuwa mwongozaji wa semina hii..






Bibie, Julie Adkins-Mshauri mwandamizi kutoka Shirika la Maendeleo la Uholanzi (S.N.V), ndiye aliyekuwa mmojawapo wa wawezeshaji wa semina hii. Hapa akitoa mifano kadhaa kwa kutumia mchoro..




Washiriki wa semina wakimfuatilia kwa ukaribu Bibie, Julie Adkins... Mpini Wa Shoka nao ulikuwa makini kwelikweli...





Mratibu wa mafunzo wa shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (S.J.M.C)-Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Abdallah Katunzi, naye pia alipata fursa kama mwezeshaji mwingine wa semina hii, japo kwa hakika muda ulikuwa mfupi mno...


No comments: