MISA-Tanzania ndani ya Arusha-February 2014.
Unaweza kuiita ni ziara ya maandalizi kwa ajili ya semina inayotarajiwa kufanyika mwezi ujao (March-2014) mjini Arusha. Ziara hii ilikuwa ni kwa ajili ya kuvifikia vyombo mbalimbali vya habari vya Arusha pamoja na vyuo vya taaluma ya habari ili kujua ni wapi hasa vilipo katika mji huu, ualisia wa kiutendaji, pamoja na mambo mengine mengi tu muhimu ya kitaaluma. Mpini Wa Shoka ulikuwa bega kwa bega ndani ya ziara hii ili kuhakikisha shabaha inafanikiwa. Baadhi ya maeneo ambayo ziara hii ilitufikisha ni katika Chuo cha Uandishi wa habari cha East African College kilichopo maeneo ya Mianzini, Triple A Fm Radio iliyopo maeneo ya Technical (jirani na chuo cha ufundi Arusha), JR institute of Technology kilichopo Sakina, Chuo cha Uandishi wa habari cha AJTC-Arusha Journalism Training College kilichopo maeneo ya kuelekea kwa Mromboo jirani na Fid Fos-Arusha (Field Force Unit), Radio Safina jirani na Florida(Kaloleni), Gazeti la Arusha Times-Safari Hotel, pamoja na Habari Maalum ambao pamoja na kuwa na kituo cha Radio ya dini (Radio Habari Maalum), lakini pia wana Chuo cha Uandishi wa habari pamoja na uzalishaji wa vipindi vya Radio, Tv na uchukuaji wa picha za video kwa matukio kadhaa ya kawaida ndani ya jamii...
Huyu ndiye Bwana Andrew Marawiti kutoka Misa-Tanzania-Media Institute of Southern Africa (Taasisi ya vyombo vya habari Kusini mwa Afrika), ambaye alisafiri kutoka jijini Dar es Salaam yalipo makao makuu ya Misa kwa hapa Tanzania, na kufika mjini Arusha kwa ajili ya ziara hiyo, ambapo Mpini Wa Shoka ulikuwa pamoja naye mguu kwa mguu... Na hapa ni wakati tulipotembelea Habari Maalum-mwendo wa kama km 15 hivi kutoka katikakati ya Mji wa Arusha kama unaelekea Namanga (barabara kuu ya Nairobi-Arusha)
...baada ya kukamilisha kukutana na wahusika wa Habari Maalum, hapa akijidai kwenye maeneo ya mojawapo ya majengo ya chuo chao.
Jua lilikuwa kali, lakini haidhuru kitu. Akapata picha moja ya ukumbusho, kisha tukaondoka zetu kurudi Arusha mjini. Ilikuwa ziara tamu na ya aina yake... Tunashukuru tuliifanikisha vema...
No comments:
Post a Comment