Nikiwa bado Mtwara, kwenye nyumba moja ya wageni niliyokuwa nikilala nililiona tangazo hili sehemu ya mapokezi (reception). Siku moja nikaamua kumuuliza kirafiki tu jamaa wa mapokezi (mhudumu):- "Eti, swahiba, haya maelekezo kwenye hili tangazo lenu hapa ukutani, ni kweli huwa mnayazingatia kama yanavyosomeka? " Mhudumu alicheka kidogo, halafu alinijibu, "unajua hizi kazi bwana zina ugumu wake. Wakati mwingine tunalizingatia; lakini wakati mwingine wateja ni wachache sana, kwa hivyo inakuwa vigumu kwa kiasi fulani..."
No comments:
Post a Comment