HAYA BADO NI MAMBO YA EID MUBARAK... EID el FITR......Baadaye nikachepukia kwenye viwanja vya michezo ya watoto. Nikatua kwenye eneo la Bwana Joseph Shirima, almaarufu Matokeo A.K.A mwanangu, vilivyopo mtaa wa Jamhuri ambapo pia kuna kituo maarufu cha kuoshea magari (Jamhuri Carwash). Hapo napo ilikuwa ni hekaheka tupu za kucheza na kusherehekea.....


Ni utitiri wa watoto, wakubwa kwa wadogo, kutoka pande mbalimbali za vitongoji na mitaa kadhaa ya Mji wa Arusha wakiwa wamejumuika pamoja katika kituo hiki cha michezo....





Hawa wakiwa katika mchezo wa mabembea...



 

Wengine wakiwa ndani ya Helkopta! Mambo ni juu kwa juu, mwanawane....





...hawa wao walikuwa katika kuendesha farasi.





Hii ndio ilikuwa kali kuliko. Hapa hata namna ya kuchukua picha ilikuwa ni kazi. Hili dude lilikuwa limejaa watoto kibao! Halafu lilipowashwa lilikuwa linakwenda kasi siyo mchezo. Picha yenyewe si unaona jinsi nilivyoinasa kwa tabu! Yaani jinsi lilivyokuwa likizunguka, kwa watoto kwao ilikuwa ni raha tupu...

No comments: