HEKAHEKA, FURAHA NA BURUDANI ZA EID EL FITR...Ili kujiepusha na usherehekeaji unaoendana na vitendo vya kumkosea Mwenyezi Mungu, waislamu wa eneo la Kata ya Daraja II-Arusha City waliamua kujumuika pamoja kwenye viwanja vya shule ya msingi Daraja II kwa ajili ya michezo mbalimbali. Pamoja na michezo mingi iliyokuwa imeandaliwa kwa wazee na vijana, lakini Mpini Wa Shoka ulibahatika kuunasa huu; mchezo wa kuvuta kamba. Wee acha. Ilikuwa ni raha na burudani ya kukata na shoka...


Ni wakati wa maandalizi. Hapa ulikuwa ni mpambano wa kuvuta kamba kati ya vijana wa msikiti wa Taqwa na wale wa msikiti wa majirani zao; Masjid Mun'nawara (msikiti wa kwa Mzee Rajabu)





Mashabiki na washangiliaji walikuwa wamefurika kila upande wakishuhudia...



 

Matayarisho na uhakiki wa waandaaji bado unaendelea ili kuuthibitisha ubora wa kamba....




Wakina mama na watoto nao pia walikuwepo tele...




Haya sasa! Mambo yameiva. Jamani, timu zote mbili mko tayari... "Ndiyooooooo, tuko tayari". Haya kila mmoja aikamate vema kamba.... moja! Mbili! Tatu..... 




...haya twende! Vuta! Vuta! Nikuvute!




Ustaadh acha kutegea. Umoja ni nguvu. Vuta! Kazana! Kazana! Vuta nikuvute... Ooooop!




Mwamuzi katikati (mwenye kanzu na kilemba) anainua mikono juu kuashiria tayari mshindi amepatikana.... Ndiyo! Mshindi amepatikana....





Mikono juu ikishangilia ushindi. Vijana wa Masjid Mun'nawara (msikiti wa kwa Mzee Rajabu) ndio washindi kwa kuishinda timu ya vijana wa msikiti wa Taqwa. Ilikuwa ni vuta nikuvute tamu na ya aina yake...

 

"Mpini Wa Shoka unawapa hongera nyingi wabunifu na waandaaji wa michezo hii. Hongereni sana..."

No comments: