EID MUBARAK...Waislamu katika maeneo mbalimbali duniani walijumuika ndani ya nyumba za ibada na hata kwenye viwanja vya wazi kwa ajili ya sherehe za Sikukuu ya IDD baada ya kuukamilisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.....
Hapa ni katika mojawapo ya misikiti ya Mji wa Arusha. Waumini baada ya kukamilika kwa swala ya Idd...
...lakini burudani kubwa ya Mpini Wa Shoka ni pale tu swala inapohitimishwa, basi msukumano mkali hutokea kwenye milango ya kutokea nje ya misikiti huku kila mmojawao akiwa amekamatia mkononi viatu vyake, malapa (kandambili) au makobazi kama ishara kwamba haraka ni kubwa mno ya kuwahi kule tunakokimbilia...!
Lakini baada ya kutoka nje, mshangao ni kwamba wengi wao hubaki wakiwa wamesimama tu hapa na pale kwa mazungumzo au majadiliano haya na yale! Sasa ule msukumano milangoni wa kutaka kutoka kwa haraka nje ya msikiti huwa ni wa nini hasa! Lakini yote heri tu.
Na kuanzia muda wa asubuhi na kuendelea hadi mchana, mambo kila mahali yalikuwa ni raha tupu. Ni kupiga vitu kwa raha na furaha zote. Mpini wa Shoka na maswahiba zake, Omari (Osama) na Freddy nao pia hawakuwa nyuma katika mpango mzima wa 'kukung'uta vintu'. Paja za kuku na vipapatio kama kawa...
No comments:
Post a Comment