ASILI YA MTOTO YOYOTE YULE, HUWA NI FURAHA NA RAHA TUPU, NA HASA PALE MATUMBO YAO YANAPOKUWA 'yameshiba vema kwa msosi', NA TENA WAWE NI WAZIMA WA AFYA TELE. MZAZI UWE NA PESA MFUKONI, AU USIWE NAYO ' uwe umechacha vilivyo', KWA WATOTO KAMA HAWA KWAO SIYO KITU KINACHOWAHUSU. WEWE UTAJUA MWENYEWE NA MAMBO YAKO; WAO WANACHOKITAKA NI MSOSI TU PALE NJAA INAPOWAUMA!
Jicho langu liliwanasa watoto hawa wawili wakiwa ndani ya furaha ya kutosha maeneo ya Kata ya Daraja II-Arusha Town. Amini usiamini hawa ni mtu na mjomba wake! Aliyekaa kulia (cheupe) anaitwa Hussein Mohammed Hussein Dudu. Na Bwana mkubwa aliyekaa kushoto akiwa katika tabasamu kali la Mpini Wa Shoka anaitwa Hashir Khamis Natoro. Bwana Hashir ni mtoto wa dada yake na (cheupe) Hussein! Kama hautaki, basi kalagabao! Hapa ishu siyo umri wala ukubwa; ishu ni heshima tu.
IDD MUBARAK KWA WATOTO WOTE KOTE DUNIANI.
No comments:
Post a Comment