...ETI WAKWETU, kati ya familia hizi mbili, ni ipi unayoiona ni yenye nafuu kidogo kama ndiyo ingekuwa ni familia yako? ....Familia hizi zote mbili zinaishi jirani kabisa na nyumbani kwako. Kwa ufupi, ni majirani zako... (1) Familia ambayo kila usiku unapokuwa unajiandaa kutaka kulala, ghafla tu unaanza kuyasikia mayowe na kilio kikubwa cha mwanamke (mke) akiomba msaada kutokana na kipigo (kifinyo kikali) kutoka kwa mumewe; na asubuhi wanapoamka, mara zote mke huwa haoneshi kabisa kujuta wala kuwa na mpango wowote ule wa kuachana na huyo jamaa'ake, Mr. Night boxer...! (2) Familia ambayo wakati wote, na hata mara nyingine kwa macho yako umekuwa ukishuhudia waziwazi, mwanamume (mume) akiperekwa mbio (akiperekeshwa vilivyo) kwa manyanyaso na masimango yasiyokuwa ya kawaida kutoka kwa mkewe; lakini hata siku moja huyo mwanamume hataki ushauri wala kusikia lolote lile, hata kutoka kwa marafiki zake wakubwa, kuhusiana na maisha yake na hicho kipusa (kipenzi) chake cha roho....!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment